June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam yarudi kileleni, yaifumua Mtibwa 5-2

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia moja ya bao walilofungwa katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar

Spread the love

MABINGWA watetezi, Azam FC wamefanikiwa kurejea kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichakaza Mtibwa Sugar kwa mabao 5-2 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Anaripoti Erasto Stanslaus …. (endelea).

Kwa ushindi huo, Azam FC imewaondoa kileleni Yanga kwa kufikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 13, sawasawa na Yanga lakini wamezidiwa wastani wa mabao.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Kipere Tchetche dakika 18 na 86, Frank Domayo dakika 26 na 58 na Didier Kavumbangu.

Mtibwa Sugar walipata mabao yao kupitia kwa Mussa Nampaka dakika ya 34 na Ame Ally aliyefungwa bao la pili dakika ya 70.

 

 

error: Content is protected !!