August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam yamshusha kocha wa Raja Casablanca

Kocha mpya wa klabu ya Azam (Kushoto), akiwa na Saad Kawemba

Spread the love

HATIMAYE klabu ya Azam Fc imeingia mkataba wa miezi sita na Aristica Cioba 45, raia wa Romania kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya siku chache zilizopita kumtimua kazi aliyekuwa mkufunzi wao Zeben Hernandez na wasaidizi wake wote kutokana kuwa na mwenendo mbaya wa timu katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Kocha huyo atasaidiwa na makocha wazawa, Idd Nassor Cheche na kocha wa makipa Idd Abubakar ambao mpaka sasa wanaiongoza timu hiyo kwenye michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar iliyofikia hatua ya nusu fainali.

Cioba ambaye alipitia katika klabu kama Raja Casablanca na Al- Masry kama kocha msaidizi kabla ya Machi 7, 2016 kujiunga na klabu ya Aduana Stars inayoshiriki ligi kuu nchini Ghana kama kocha mkuu wa timu hiyo.

Majukumu ya kocha huyo mpya yataanza mara baada ya kukamilika kwa vibari vyake vya kufanyia kazi nchini, lakini kwa sasa ataenda visiwani Zanzibar kuangalia mwenendo wa timu ulivyo na ataendelea kutoa ushauri panapo hitajika lakini hatoweza kukaa kwenye benchi.

error: Content is protected !!