KAMPUNI ya Azam Media, wamekuja na mradi wa kufunga taa kwenye viwanja vinne vinavyochezewa Ligi kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)
Lengo la mpango huo ni, kuondoa mechi zaa saa 8 mchana ambazo zinawanyima watu wengi fursa za kutazama mpira kutokana na kuwa kwenye shughuli zao za kila siku.
Viwanja ambavyo vitakuwa sehemu ya mradi huo ni Uwanja wa Majaliwa ulipo Lindi unaotumia na Namungo FC na uwanja wa Kaitaba uliopo Kagera unaotumia na Kagera Sugar.
Vingine ni, Mkwakwani jijini Tanga unaotumia na Costal Union pamoja na Uwanja wa Gwambina ulipo Mwanza, unaotumiwa na Gwambina FC.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne tarehe 16 Februari 2021, kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam, mwakilishi kutoka Azam Media, Mhandisi Ndozero amesema, mradi huo umezingatia sehemu nzuri ya kuchezea (Pitch) na mazingira yote ya uwanja.
“Tuna kila sababu ya kuhakikisha mradi huu unakwenda kama, sisi tumejitahidi kufuata utaratibu wote unahitajika, na lengo kubwa ni kuepukana na mechi saa 8 mchana kwa kuwa zinaumiza kwani kuna nyakati haziepukiki licha ya bodi ya Ligi kujitahidi,” amesema
“Michakato utakapo kamilika bodi ya Ligi watakuwa na nafasi ya kupanga mechi kuchezwa muda wote kuanzia saa 1 usiku na mantiki hiyo tutapata picha zilizo bora” amesema Ndozero
Aidha, Ndozero amesema, sababu za zimesababisha biashara zimesababisha kuamua kufunga taa kwenye viwanja hivyo ili watu wengi waliolipia ving’amuzi vyao waweze kutaza michezo mingi zaidi katika muda mzuri.
Amesema, toka kuanza kwa msimu huu Azam TV imeonesha idadi kubwa ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya mechi nyingi kuonekana ukitofautisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Leave a comment