August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC yawasambaratisha Wasauzi

Spread the love

AZAM FC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuiadhibu Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3, mchezo uliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Azam imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7-3 baada ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Afrika Kusini.

Mabao ya Azam yalifungwa na Kipre Tcheche aliyefunga matatu (hat-trick) katika dakika 22, 55, 88 huku nahodha wake, John Bocco akifunga dakika 42.

error: Content is protected !!