July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC yashusha kifaa kutoka Zambia

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Azam FC, imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Charles Zulu raia wa Zambia, aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Cape Town City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kiungo huyo amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao 2021/22, ili kuimalisha kikosi cha kilichopo chini ya kocha George Lwandamina kutoka Zambia.

Azam FC, wanafanya usajili huo wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa mwishoni, ambapo wakati msimu huu unaanza kikosi hiko kilifanikiwa kushinda michezo saba ya mwanzoni.

Usajili wa mchezaji umethibitishwa kupitia kurasa rasmi kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ambapo ilimuonesha mchezaji huyo akisaini mkataba akiwa pamoja na Afisa mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdukarim Amin ‘Popat’

Zulu kabla ya kutumika kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini, alitokea kwenye klabu ya Zanaco FC ya Zambia, ambao ni vigogo wa soka wa nchini humo.

Klabu hiyo imeshaanza kufanya usajili ikiwa bado haijafahamika tarehe halisi ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili, kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Azam FC wanaungana na Yanga kufanya usajili mapema, kufuatia timu hizo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa msimu ujao, itakayoanza tarehe 12 Septemba, 2021, na hivyo klabu hizo kuwa na muda mchache wa maandalizi.

Yanga mpaka sasa imefanikiwa kunasa saini ya mlinzi wa kulia wa klabu ya As Vita ya nchini Congo Djuma Shaban ambaye siku chache zijazo atatua nchini.

error: Content is protected !!