June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam Fc yasaini mwengine kutoka Congo

Spread the love

KLABU ya Azam FC imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji raiawa kidemokrasia ya Congo, Idris Mbombo kwa mkataba wa miaka miwili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezaji huyo amesaini mkataba huo, mbele ya mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdukarim Amin ‘Popat’ leo jijini Dar es Salaam.

Mbombo ambaye amepita kwenye klabu za Nkana Red Devil na Zesco zote kutoka Zambia na baadae kukipiga kwenye klabu ya Kabwe Warriors na kisha kutimkia nchini Misri kwenye timu ya Al Gouna.

Mshambuliaji huyo, anatimiza idadi ya wachezaji sita waliosajiliwa na klabu hiyo mpaka sasa kuelekea msimu ujao wa mashindano.

error: Content is protected !!