July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC yaendelea kusajili kimyakimya

Spread the love

 

TIMU ya Azam FC ya Chamanzi, Tanzania imeendelea kukisuka kikosi chake cha msimu ujao wa 2021/22, kwa kusajili wachezaji wanne wa Kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Azam FC imemaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2020/21 huku Simba ikitetea ubingwa wa ligi hiyo mara nne mfululizo.

Vijana hao wa Chamanzi, wanakisuka kikosi chao ambao msimu ujao, kitaungana na Biashara United ya mkoani Mara, kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tayari Azam amekwisha wasainisha wachezaji watatu kati yao yumo Edward Manyama, raia wa Tanzania akitokea Ruvu Shooting.

Manyama, ambaye ni beki wa kushoto wa timu ya Taifa, amesajiliwa kwa mkataba huru wa miaka miaka miwili utakaomwezesha kukaa Chamanzi hadi mwaka 2024.

“Manyama ni mmoja wa mabeki wa kushoto wanaoendelea kufanya vizuri kwenye ligi yetu, ingizo lake ndani ya kikosi chetu ni katika kuimarisha zaidi eneo hilo,” imeeleza taarifa ya Azam.

Leo Jumatano, tarehe 21 Julai 2021, imemtambulisha kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna.

Maguna amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya. Mchezaji huyo amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Kombe la FA nchini humo, huku Gor Mahia ikiibuka mabingwa wa michuano hiyo.

Azam imesema “Muguna anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu kwenye eneo la ushambuliaji, mkataba huo utamfanya kuitumikia Azam FC hadi mwaka 2023.”

Mwingine aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ni mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco ya huko pamoja na kiungo kutoka Zambia, Charles Zulu.

Aidha Kola ambaye wakala wake ni Nir Karin, akiwa Zanaco msimu uliopita, alifunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.

error: Content is protected !!