Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Azam FC yabanwa mbavu Mkwakwani, Mtibwa mambo magumu
Michezo

Azam FC yabanwa mbavu Mkwakwani, Mtibwa mambo magumu

Spread the love

 

Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara limefunguliwa rasmi hii leo Septemba 27, 2021 kwa kupigwa jumla ya michezo mitatu kwa kuchezwa michezo mitatu katika viwanja tofauti hapa nchini. Anaripoti Damas Ndelema TUDARCo (endelea)………

Pazia hilo limefunguliwa kwa mechi ya mapema ambao ulipigwa majira ya Saa 8:00 mchana kwa kuzikutanisha klabu ya Mtibwa Sugar  iliyokua mwenyeji dhidi ya Mbeya kwanza kutoka Jijini Mbeya ambao wqalifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0.

Bao pekee la Mbeya Kwanza kwenye mchezo huo lilifungwa na Willy Edgar katika Dakika ya 49 na kuweka rekodi ya kufunga bao la kwanza kufungwa msimu huu 2021/22.

Kwa upande wa Azam FC ambao walishuka dimbani majira ya saa 10 jioni kwenye uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union na kulazimishwa sare ya bao 1-1.

Kwenye mchezo huo Azam FC ilikuwa ya kwanza kupata bao kwenye dakika ya 49, kupitia kwa Daniel Amoah, huku bao la kusawazisha la Coastal Union ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo likifungwa na Hance Masoud kwenye dakika 90 ya mchezo.

Namungo wao wakiwa kwenye dimba la nyumbani mkoani Lindi kwenye Uwanja wa Majaliwa, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Geita Gold ambayo inacheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza toka ilipopanda daraja.

Mabao ya Namungo kwenye mchezo huo yalifungwa na Shiza Kichuya kwenye dakika ya 13 na Reliant Lusajo dakika ya 81 na kuifanya timu hiyo kukaa kileleni kwenye msimamo.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa jumla ya michezo mitatu, ambapo mabigwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara  klabu ya soka ya Simba itakua ugenini dhidi ya Biashara United ya mkoani  Mara katika dimba la  Karume Stadium  majira ya saa 10 jioni.

Michezo mingine itakuwa ni Dodoma Jiji dhidi ya Ruvu shooting na Mbeya city itamenyana na Tanzania Prisons kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!