May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC yaanza kujinoa Zambia

Spread the love

 

KLABU ya Azam imeanza mazoezi yake ya maandalizi ya msimu ujao 2021/22 katika kambi iliopo mji wa Ndola nchini  Zambia. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo…(endelea)

Klabu hio iliondoka nchini Tanzania jana jumatatu ya Agosti 23, 2021 kuelekea nchini Zambia kisha kupumzika na kuendelea na mazoezi siku ya leo jumanne.

Kikosi hicho kilitarajia kuondoka na jumla ya wachezaji 28 lakini kimeshindwa, na kuamua kuondoka na wachezaji 19 kutokana na wachezaji wao 7 kuitwa timu ya taifa huku wachezaji wawili wakiwa ni majeruhi.

Wachezaji ambao ambao wamekosa kambi hiyok kutokana na majeruhi ni nahodha wa kikosi hiko Agrey Moris na Wilbroad Maseke.

Kwa upande wa Prince Dube yeye atajiunga na timu hiyo musa wowote kutoka sasa na kukamilisha idadi ya wachezaji 20.

Taarifa ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji hao ilithibitisha na Zacharia Thabiti ambae ni mkuu wa idara ya habari na Mawasiliano ya klabu hiyo ambaye alisema kuwa wachezaji hao watakosekana kutokana na sababu hizo huku akitanabaisha kuwa Prince Dube atajiunga na wenzake muda wwote kutoka sasa.

“Tulitarajia kuondoka na wachezaji 28 lakini imeshindikana kutokana na wachezaji walioitwa na timu zao za taifa ambao ni saba pia wachezaji wawili ni majeruhi ambao ni wilbroad maseke na Agrey Moris lakini prince atawasiri kambini kujumuika na wachezaji wenzake na kufika jumla ya wachezaji 20’’alisema Zacharia.

Katika kambi hiyo nchini Zambia, Azam FC itacheza michezo ya kirafiki na klabu za Zanaco, Zesco na Forest Rangers.

Kwa upande wa mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdukharim Amin ‘Popat’ alisema kuwa michezo hiyo ya kirafiki itachezwa kila baada ya siku mbili na kufunguka kuwa vibari vya kimataifa kwa wachezaji waliowasajili kutoka nje ya nchi vimeshakamilika.

“Kwa mujibu wa programu ilivyo, tutaanza kuwa na mechi kila baada ya siku mbili mpaka siku ya kurudi tunategemea kuwa na mechi tatu na vibari vya wachezaji tayari tumeshavipata.” popat.

 

error: Content is protected !!