August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam Fc yaachana rasmi na makocha wake

Zeben Hernandez katikakati akiwa na wasaidizi wake

Spread the love

BAADA ya taarifa zilizoenea jana juu ya klabu ya Azam Fc kuachana na jopo la makocha wao raia wa Hispania, wakiongozwa na kocha mkuu  Zeben Hernandez na wasaidizi wake, hatimaye uongozi wa klabu hiyo umetoa taaarifa rasmi juu ya kuachana na benchi hilo la ufundi, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Katika taarifa hiyo uongozi wa klabu ya Azam Fc umesema umefikia makubaliano kwa pande zote mbili ya kusitisha mikataba kwa makocha hao kuendelea kuifundisha timu hiyo kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri wa timu.

Maamuzi hayo yamefikiwa na bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo jana, kutokana na kupata matokeo mabovu kwenye ligi kuu, baada ya kucheza michezo 18 na kufanikiwa kushinda nane, sare sita na kufungwa michezo minne na kushika nafasi ya nne kwenye ligi.

Kwa sasa uongozi wa klabu hiyo upo katika mchakato wa kusaka Mwalimu mpya, huku jina la kocha Kali Ongala ambaye anayeifundisha timu ya Majimaji kwa sasa likitajwa kwenda kuchukua mikoba ya wahispania hao lakini kwa sasa kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha wa timu ya vijana  Iddi Cheche na kocha wa makipa Iddi Abubakar kwa kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

Zeben anakuwa kocha wa tisa kutimulia ndani ya klabu ya Azam Fc katika kipindi cha miaka tisa toka ilipo anza kushiriki ligi kuu, huku ikifanikiwa kutwaa ubingwa mara moja tu chini ya kocha Joseph Omog ambaye anakinoa kikosi cha Simba kwa sasa.

error: Content is protected !!