May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC wampa mkataba mpya Dube mpaka 2024

Spread the love

Klabu ya Azam Fc imemuongezea mkataba miaka miwili mshambuliaji wake raia wa Zimbabwe Prince Dube ambapo utamfanya kusalia hapo hadi 2024. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Dube amesaini mkataba huo hii leo tarehe 1 Juni, 2021 mbele ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo Abdukarim Amin maarufu kama Popat.

Mshambuliaji huyo kwa sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mara baada ya kuingia kambani mara 17.

Mfumania nyavu huyo  alijiunga na Azam FC mwezi Agost 2021 kwenye dirisha kubwa la usajili.

error: Content is protected !!