May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam Fc, Simba dimbani leo

Spread the love

 

Robo fainali ya tatu nan ne zitaendelea tena hii leo kwenye viwanja tofauti, ambapo Jijini Dar es Salaam mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Simba itashuka Uwanjani kumenyana na Dodoma jiji FC kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku Azam Fc atakuwa ugenini mkoani Tabro dhidi ya Rhino Rangers. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo utakaotangulia utakuwa wa Azam FC ambao utachezwa majira ya saa 10 jioni, na kufuatia na mchezo wa Simba dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaopigwa majira ya saa 1 usiku.

Clatous Chama, kiungo wa klabu ya Simba

Washindi katika michezo hii miwili ya leo watakutana kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Prince Dube

Tayari Yanga imeshafuzu kwenye nusu fainali mara baada ya kuifunga Mwadui FC kwa mabao 2-0, na ambapo kwenye mchezo wa nusu fainali atavaana na Biashara United ambayo iliwaondosha Namungo FC.

error: Content is protected !!