May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Azam Fc, Mwadui Dimbani leo

Spread the love

LIGI kuu Tanzania Bara itaendelea tena leo kwa jumla ya michezo miwili kupigwa kwenye viwanja tofauti ambapo klabu ya Azam Fc itashuka dimbani kwenye mchezo wake wa sita wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui Fc kutoka Shinyanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi huku Azam Fc itamkosa beki wake Yakub Mohamed ambaye amechelewa kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ya Ghana.

Mchezo mwengine utaikutanisha timu ya Gwambina Fc ambao watatumia Uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya kufungiwa na bodi ya Ligi kwa kuikaribisha Mtibwa Sugar kutoka Morogoro

Mpaka sasa Azam Fc wapo kileleni kwenye msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 15 mara baada ya kucheza michezo mitano, huku wakifuatiwa na klabu ya Simba yenye pointi 13 sawa na Yanga ambao wanashika nafasi ya tatu.

error: Content is protected !!