August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC kuivaa Mtibwa kombe la FA

Ratiba ya raundi ya sita ya ASFC

Spread the love

KLABU ya Azam FC itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar, katika raundi ya tano ya kombe la Shirikisho (FA) mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Azam Complex uliopangwa kufanyika 24 Febuari 2017 baada ya ratiba kutoka leo, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Katika michuano hiyo zilizobaki timu 16, na baada ya kuamaliza michezo hii ya raundi ya tano itakwenda katika hatua ya robo fainali, baada ya kubakia timu nane.

Michezo mengine itakayopigwa tarehe kama hiyo ni Kagera Sugar dhidi ya Stand United, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, huku Mighty Elephant kutoka mkoani Songea itapambana na Ndanda FC katika uwanja wa Majimaji na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Madini kutoka Arusha na JKT Ruvu.

Aidha ratiba hiyo itaendelea tena tarehe 26 Februari mwaka huu, mchezo wa kwanza utawakutanisha Mbao FC dhidi ya Toto Africans, kwenye Uwanja CCM Kirumba na mchezo wa pili utakuwa kati ya Tanzania Prison ambao watawakabili ndugu zao Mbeya City mchezo utaochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Naye bingwa mtetezi wa kombe hilo, Yanga, itaivaa timu ya Kiluvya United ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza, mchezo uliopangwa kufanyika tarehe 7 Machi 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, huku mahasimu wao Simba watawakaribisha timu ya African Lyon, mechi iliopangwa kufanyika tarehe 1 Machi.

error: Content is protected !!