Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Azaki zatakiwa kulinda haki za wanawake
Habari Mchanganyiko

Azaki zatakiwa kulinda haki za wanawake

Spread the love

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kulinda na kutetea haki za wanawake Tanzania (Tasuwori) imezitaka Azaki zote nchini kuungana na kuwa na sauti moja kwa kusemea sera kandamizi zinazoumiza wananchi ili ziweze kubadilishwa na kuleta manufaa kwa Umma, anaandika Christina Haule.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tasuwori, Emmanuel Mapigano amesema kwenye mafunzo ya ushawishi na utetezi yaliyohusisha Azaki za kiraia na watendaji wachache kutoka serikalini yaliyofadhiliwa na ubalozi wa Ufaransa chini ya mradi wao wa PISCA na kufanyika mkoani Morogoro.

Mapigano amesema kuwa ikiwa Azaki zote nchini zitakuwa na sauti moja na kutumia dhana ya ushawishi na utetezi usioathiri pande mbili yaani Azaki na serikali zitaweza kupiga hatua kubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii zikitumia mbinu bora za kitafiti ili kuujua ukweli na kuwa na ushahidi wa kutosha kabla ya kufikisha utetezi wao kwenye vyombo husika ili kusiwe na tofauti katika pande hizo.

“Kutokuwa na ushawishi na utetezi uliozingatia utafiti na ushahidi wa kujitosheleza ikiwemo picha, kumeweza kuleta shida katika azaki kadhaa na watendaji wake kuchukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani, hivyo Azaki ni muhimu kuwa na tafiti sahihi na ushahidi kamili,” amesema.

Naye Frank Luvanda ambaye ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Asasi za Mazingira Tanzania (Manet) amesema mafunzo hayo yatawasaidia wananchi katika changamoto zao kufuatia Azaki kuwa na uwezo mkubwa wa kuwatetea wananchi tofauti na Mashirika ya Kiserikali ambayo hayana uhuru wa kuwasemea wananchi hata kama wanaonewa na kubaki kutekeleza miradi na kiuchumi pekee.

Luvanda amesema kufuatia kuwa Serikali iliyopo madarakani kwa sasa ni sikivu wanaimani watafika katika hatua nzuri kwenye utetezi na kutafuta haki kwa jamii ambapo amewaasa wana Azaki wenzake kujituma.

Subira Ngonyani, Mjumbe wa Shirika la Kuwezesha Maendeleo kwa Jamii (Shimaja) amesema mafunzo hayo yamemuongezea mbinu ambapo awali aliweza kukumbana na changamoto ya mfumo dume uliomuathiri kiutendaji wakati akifanya utetezi kwa jamii.

Amesema baada ya mafunzo hayo anaamini ataweza kupaza sauti kwa jamii hasa wanawake ili kuweza kuwatetea hasa pale wanapokandamizwa na hoja kandamizi ikiwemo kushushwa na kudharauliwa hasa wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi wa ndani ya vyama vya siasa au wa kitaifa.

Joseph Pupa, Mjumbe wa Asasi ya Kuondoa Umaskini kwa Wanawake Tanzania (Wopata), amesema zipo sera zinazotumika na wakati mwingine kuwa kandamizi kwa jamii kuwa ni pamoja na ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni, migogoro ya ardhi na migogoro ya ndoa ambazo zinatakiwa kupigiwa kelele ili kuweza kuwekewa njia sahihi ya kuweza kutumika na kuwa na manufaa kwa jamii.

Lengo la mafunzo hayo ni kuona taasisi hizo zinabadili utendaji kazi wake kwa kufuata mbinu za ushawishi na utetezi huku sheria au sera zikibadilisha maudhui na umma au jamii ukibadilisha mitazamo, tabia na hulka ilizokuwa nazo awali na kuwa nazo zilizo bora kwa sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!