Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa AZAKI zang’ata na kupuliza utendaji wa JPM
Habari za Siasa

AZAKI zang’ata na kupuliza utendaji wa JPM

Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC akihutubia wajumbe wa mkutano huo
Spread the love

ASASI za Kiraia nchini (AZAKI) zimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuboresha huduma za kijamii na usimamizi wa rasilimali za Taifa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hata hivyo, AZAKI hizo zimekosoa ubinywaji wa uhuru wa vyombo vya habari na watu kujieleza, sambamba na vitendo vinavyodumaza shughuli za vyama vya siasa nchini, hasa vya upinzani.

Onesmo Ole Ngurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa  Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), amesema serikali hiyo imefanikiwa kutekeleza baadhi ya mambo yaliyoainishwa katika ilani ya uchaguzi  iliyopita, ya  AZAKI ya mwaka 2014/2015.

Ole Ngurumwa amesema hayo wakati kizungumza katika halfa ya uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Asasi za Kiraia ya mwaka 2019/2020, leo tarehe 28 Septemba 2019, jijini Dar es Salaam.

Ole Ngurumwa ametaja mambo yaliyotekelezwa katika ilani ya uchaguzi ya AZAKI ya mwaka 2014/2015, ikiwa pamoja na uboreshwaji wa elimu, huduma za afya na maji.

“Suala la elimu, ilani yetu ilisisitiza suala la elimu, serikali ya awamu hii tumeona mambo mazuri yamefanyika katika eneo la jamii hasa elimu bure. Kuboresha huduma za afya, mfano katika vijiji kuna zahanati, vituo vya afya vimeongezeka mara dufu,” amesema Ole Ngurumwa .

Pia, Ole Ngurumwa amesema serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na kusimamia rasilimali za taifa.

“Tumeona asilimia kubwa, jitihada za wazi kuhakikisha rasilimali za nchi zimeweza kulindwa ingawa kuna changamoto nyingi. Lakini jitihada zimeonekana kulinda malighafi, madini na wanyamapori. Hili lilikuwa takwa letu, lakini limefanyiwa kazi kwa kiwango cha kuridhisha,” amesema Ole Ngurumwa na kuongeza;

“Suala la rushwa nalo limefanyiwa kazi, mapato tumeona yamekusanywa mpaka kupitiliza hadi watu wanaumia. Ilikuwa takwa letu kodi likusanywe.”

Ole Ngurumwa ameeleza kuwa, serikali imeonesha nia ya kuleta maendeleo, kwa kuanzisha mikakati mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda na miundombinu.

“Kwa ufupi hayo mambo tumeona. Mipango ya maendeleo, mikakati ya viwanda imeonakana tayari ni mafanikio. Barabara za rami. Ni sehemu ambazo zinaweza chagiza maendeleo. Hayo nimetakwa yetu yamefanyiwa kazi inaridhisha,” ameeleza Ole Ngurumwa.

Hata hivyo, Ole Ngurumwa amesema katika Serikali ya Awamu ya Tano imeshuhudiwa changamoto ya uhuru wa vyombo vya habari, watu kujieleza pamoja na wanasiasa kubanwa kufanya shughuli zao.

“Suala la uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari tulieleza kama takwa letu, lakini ninyi mashahidi. Takwa hili limeendelea kuwa changamoto. Uhuru wa Watanzania kufanya shughuli zao mbalimbali na kujieleza, wanasiasa kubanwa. Utungwaji wa sheria za kubana wanasiasa asasi za kiraia,” amesema Ole Ngurumwa na kuongeza;

“Bado changamoto kubwa tunaona kwenye chaguzi zinazokuja zifanyiwe kazi. Haki za binadamu, utawala bora, masuala ya kuheshimu tunu na utu wa mtu. Vyote vinakwenda kwenye suala la kusuasasua, bado tunatatizo la kuheshimu haki za watanzania na utawala bora.”

Akizungumzia kuhusu ilani ya uchaguzi ya AZAKI ya mwaka 2019/2020, Israel Ilunde ametaja mambo kumi ambayo wadau wa asasi za kiraia wanapendekeza yafanyiwe kazi na viongozi watakaochaguliwa kwenye chaguzi zijazo.

Jambo la kwanza ni ulinzi wa haki za binadamu na utawala bora, la pili ni ukatiba, la tatu uchumi jumuishi na endelevu, na la nne, ni Ulinzi na usimamizi wa rasilimali za umma.

Jambo la tano ni, usawa wa kijinsia na makundi maalumu, wakati la sita likiwa ni upatikanaji na unafuu wa huduma za msingi za kijamii, huku la saba likiwa ni amani, usalama, umoja na mshikamano wa Taifa.

Ilunde amesema jambo la nane, ni Tanzania na Diplomasia ya Kikanda na Kimataifa, wakati la tisa likiwa ni uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukutana. Huku la mwisho likiwa ni uwekezaji na ulinzi wa matumizi ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!