July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

AZAKI zalia na hali ya kisiasa Zanzibar

Spread the love

ASASI za kiraia zimewataka viongozi wakubwa kutumia siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa taarifa fafanuzi inayojibu ajenda zao, kueleza walipofikia katika majadiliano yao ya kutatua mgogoro wa urais Zanzibar. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yameelezwa katika tamko lao jana kufuatia ukimya unaoendelea kuhusu suala la mgogoro uliotokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar 25 Oktoba kufutwa na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Akizungumgumza na Waandishi wa habari Mratibu wa Kitaifa-Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa na Katibu Mkuu-Braza la Taifa la Asasi za Kiraia (NACONGO), Deus M Kibamba.

Wameeleza kuwa viongozi hao wafanye utatuzi wa mgogoro huo kwa kuzingatia misingi ya katiba ya Zanzibar ya 1984, toleo la 2010, pamoja na sheria ya uchaguzi ya Zanzibar namba 11. ya 1984.

“Tunasema hilo kwa kuamini kuwa upatikane muafaka ambao utakubalika kisheria kwa maana ya kuwa hautafikiriwa kuhojiwa mbele ya sheria.” Imeelezwa katika tamko hilo.

Asasi hizo zimewatala viongozi wote watumie siku ya mapinduzi ya Zanzibar kueleza wananchi hatma ya Zanzibar kisiasa kwa kuwa mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya juu ya mambo yanayomuhusu yeye na taifa lake.

Walieleza kuwa wananchi walishiriki kupiga kura, sasa wana kila sababu ya kujua hatma ya viongozi waliowachagua, haki hiyo ambayo ni ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 21 (2) ya katika ya Zanzibar na inaweza kwenda kudaiwa mahakamani muda wowote.

Wanaasasi za kiraia hao wamesihi viongozi wote wa dini na wadau wa maendeleo kuingilia kati suala la Zanzibar kwani viashiria vya viongozi wakubwa kujibizana majukwani vinaweza kuendelea kujenga chuki miongoni mwa jamii.

“Tunawakumbusha vyama vya siasa viamke na kushinikiza serikali ya awamu ya tano kulipatia ufumbuzi suala la Zanzibar ili wananchi waweze kuendelea shughuli zao za kila siku.” Imeeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!