Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko AZAKI wajinoa kutekeleza mapendekezo 187 ya UN
Habari Mchanganyiko

AZAKI wajinoa kutekeleza mapendekezo 187 ya UN

Spread the love

WADAU wa Asasi za Kiraia (AZAKI), wameandaa mpango mkakati wa utekelezaji mapendekezo 187 ya Umoja wa Mataifa (UN), ambayo Serikali ya Tanzania, imekubali kuyatekeleza kupitia mchakato wa mapitio ya hali ya haki za bunadamu (UPR). Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro…(endelea).

Mpango huo umeandaliwa katika kikao kazi cha AZAKI cha kupitia mapendekezo hayo, kilichofanyika mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki iliyopita. Kikao hicho kiliandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD).

Afisa Uchechemuzi THRDC, Nuru Maro amesema mpango kazi huo umeanisha maeneo muhimu tisa, ikiwemo ya haki za binadamu katika makundi maalumu ikiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

“Serikali ilipokea mapendekezo ya awali 2021 na kupokea ya mwisho Machi 2022, tulipokea mapendekezo 187. Kati yake 167 yakiwa yamekubaliwa moja kwa moja na 20 yamekubaliwa kwa sehemu. Tulikutana wadau kwa ajili ya kutengeneza mpango kazi utakaotuongoza kutekeleza hayo mapendekezo,” amesema Nuru na kuongeza:

“Tumetengeneza mpango kazi ambao umeanisha maeneo muhimu tisa, ambayo asasi zitakwenda kufanyia kazi ili kitekele,a mapendeke,o haya ya UPR.”

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania, Nabor Assey, aliwaomba wadau hao kuendelea kuweka mikakati zaidi itakayowezesha utekelezwaji wa mapendekezo hayo ya UN.

“Sisi kama waday wajibu wetu kwenda kutekeleza hayo mapendekezo ambayo Serikali imekubali 187, wajibu wety kupanga mikakati ya kutekeleza kwenye maeneo yetu ya kazi kwa kutenga bajeti ili matokeo yawe chanya,” amesema Assey.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!