Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa AZAKI kuzindua ilani ya uchaguzi
Habari za Siasa

AZAKI kuzindua ilani ya uchaguzi

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu Taifa
Spread the love

ASASI za Kiraia nchini (AZAKI), kesho tarehe 28 Septemba 2019, zimepanga kuzindua ilani ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani. Anaripoti Martin Kamote… endelea).

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) amesema, uzinduzi wa ilani hiyo, unalenga kusaidia mchakato wa chaguzi hizo.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Septemba 2019 mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za THRDC jijini Dar es Salaam na kwamba, uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Kisenga uliopo kwenye jengo la LAPF, Kijitonyama.

Amesema, ilani hiyo ina vipaumbele 10 na kuwa, vina lengo la kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakwenda sawa kabla na baada.

“Tuna vipaumbele 10 kwenye ilani hiyo, kwa kuwa viongozi wa Azaki wameamua kuijenga jamii kwa kuzingatia maslahi ya uhuru na kujenga Amani, wameamua kuunda ilani hiyo.

“Ilani ya 2015 ilishaonekana ni kutoa muongozo juu ya vyama vya siasa, vyombo vya usalama, serikali na wananchi kwa ujumla ni namna gani wanatakiwa kushiriiki uchaguzi ambao utafanyika mwakani na huu serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu kwa amani na utulivu,”amesema.

Deus Kibamba, Mkurugenzi wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi amesema, kwa takribani miaka 50 Azaki zimekuwa zikifanya kazi ya kutoa elimu ya mpiga kura, elimu ya uraia na mambo ya uchaguzi katika kuangalia uchaguzi pamoja na kuainisha vipaumbele muhimu.

“Mambo yaliyopo kwenye ilani tumeyaweka ili vyama vya siasa viyabebe katika harakati za uchaguzi kuanzia kampeni hadi kukamilika uchaguzi wenyewe,” amesema.

Amesema, lengo lingine ni kutoa muongozo kwa Asasi za Kiraia ili kutekeleza majukunu yao.

“Azaki zimekuwa na mchango mkubwa katika utetezi wa haki za kijamii na utoaji wa huduma za kijamii kama vile afya.

“Tumekuwa tukiangalia pia uchaguzi ndani na nje kwa ajili ya kujifunza mambo mazuri pamoja na changamoto, haya yote yametokana na kuimarika kwa mahusiano baina ya Azaki, Serikali Kuu, Mahakama, Bunge na Jeshi la Polisi,” amesema.

Israel Ilunde, Mkurugenzi wa Ushiriki Tanzania amesema, viongozi wa vyama vya siasa ni vyema wakajitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa ilani hiyo.

Ni kwa kuwa, jambo hilo ni muhimu na wanapaswa kuchukua matakwa ya Ilani ya Azaki na kuyaweka katika ilani zao za uchaguzi.

“Viongozi wa dini waendelee kuhubiri amani kwa waumini wao na kujiepusha kutamka kauli za kuonesha kutamka zenye mwelekeo wa kupendelea mgombea au chama fulani kwenye majukwaa yao au mitaani, viongozi wa dini wanapaswa kuonya na kupaza sauti dhidi ya vitendo vya kukiuka sharia kwa viongozi wa siasa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!