Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Aweso atoa maagizo kwa watalamu wizara ya maji
Habari Mchanganyiko

Aweso atoa maagizo kwa watalamu wizara ya maji

Juma Aweso, Waziri wa Maji
Spread the love

 

WAZIRI wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amekagua mtambo mkubwa wa kuchuja maji chumvi katika eneo la Serengeti, Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro ili kujiridhisha na huduma ya majisafi inayotolewa kwa wananchi. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Aweso amefanya ziara hiyo ya kikazi leo Jumamosi, tarehe 4 Septemba 2021 kwa lengo kuu ikiwa ni kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi na salama wilayani Gairo.

Amewataka watalaamu kufanya kazi ya utafiti na kuchimba visima virefu eneo la Ngiloli ili kuongeza haraka iwezekanavyo kiasi cha majisafi kwa wananchi mjini Gairo.

Aidha ameagiza tathmini na hatua za awali zifanyike ili kuweza kutoa maji kutoka chanzo cha maji cha Chagongwe kupeleka mjini Gairo ikiwa ni mpango wa kudumu utakaomaliza changamoto ya uhaba wa huduma ya majisafi.

Waziri Aweso amesema, pamoja na hatua hizo alizoelekeza, amewataka Mamlaka ya Nishati na Maji (Ewura) kufanya kazi ya tathmini ya bei ya majisafi inayotumika mjini Gairo endapo inaendana na uhalisia wa gharama za uendeshaji ili wananchi wasiumie katika kupata huduma ya majisafi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!