Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Awamu ya Tano: Watumishi 32,555 ‘waisoma namba’
Habari za Siasa

Awamu ya Tano: Watumishi 32,555 ‘waisoma namba’

Seleman Jafo
Spread the love

JUMLA ya watumishi 32,555 wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi, kushushwa vyeo na kushushwa mishahara katika serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waliokutwa na dhoruba hizo ni wale waliobainika kuwa wazembe kazini, kughushi vyeti, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Kauli hiyo imetolewa na Rais John Magufuli leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020, bungeni jijini Dodoma, katika hafla ya ufungaji wa shughuli za Bunge la 11.

“Kama tulivyoahidi, hatutakuwa na mzaha kwa viongozi na watumishi wazembe walioshindwa kufanya kazi kwa weledi, nidhamu, maalifa na uadilifu. Waliobainika walichukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuwatumbua, kuwashusha vyeo na mishahara au kuwapa onyo kali,” amesema Rais Magufuli.

Rais wa Tanzania, John Magufuli

Kiongozi huyo wa Tanzania amesema, katika uongozi wake, watumishi 15,508 waliachishwa kazi baada ya kukutwa na vyeti vya kughushi, alifuta ajira hewa 19,708 zilizokuwa zikigharimu Sh. 19.8 bilioni na kwamba, hatua hiyo ilitoa fursa ya kaujiri watumishi wapya 74,173.

Pia amesema, serikali yake imefanikiwa kuwapandisha vyeo watumishi 306,967 na kulipa madeni mbalimbali ya watumishi kiasi cha Sh. 472.6 Bil., ambapo ya kimshahara ni Sh. 114.5 Bil., na yasiyo ya kimshahara Sh. 358.1 Bil.

Serikali ya Rais Magufuli alianza kuongoza Tanzania Novemba 2015. Serikali imetambulika zaidi kwa mtindo wa ‘kutumbua’ watumishi walioonekana kutokwenda sawia na mwendo wa serikali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!