October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aveva, Nyange wafutiwa mashtaka ya utakatishaji fedha

Spread the love

EVANS Aveva, aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba na makamu wake Godfrey Nyange, wamefutiwa mashtaka mawili ya utakatishaji fedha, kati ya mashtaka kumi yaliyokuwa yanawakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Mashtaka hayo yamefutwa leo tarehe 19 Septemba 2019 na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo.

Mahakama hiyo imeeleza kwamba, dhamana ya watuhumiwa hao iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. 30 milioni.

Aveva na Nyange kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka nane ambayo mahakama hiyo imekuta wana kesi ya kujibu.

Mashtaka hayo ni pamoja na  ya matumizi mabaya ya madaraka, kula njama, kughushi nyaraka zinazoonesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa rais huyo mstaafu wa Simba.

error: Content is protected !!