May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aucho, Fei Toto kuikosa Azam FC, Bangala Farid hati hati

Spread the love

 

VIUNGO wa klabu ya Yanga Feisal Salum ‘Fei Toto’ sambamba na Khalid Aucho hawatakuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kitakachoshuka dimbani kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa Ligi Tanzania Bara mzunguko wa pili utapigwa kesho tarehe 6 Aprili 2022, majira ya saa 2:15 kwenye dimba la Azam Complex Chamazi.

Feisal anaukosa mchezo mara baada ya wiki iliyopita kupama maumivu alipokuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa na kupewa mapumziko ya siku 14.

Akitoa taarifa juu ya wachezaji hao, kocha msaidi wa klabu ya Yanga Cedric Kaze aliwaambia wanahabari kuwa viungo hao wawili hawatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho.

“Kuna wachezaji ambao tutawakosa kwenye mchezo wa kesho Aucho, Feisal wao bado wanauguza majeraha yao, kutokana na kuumia .” Alisema kocha huyo.

Kwa upande wa Yanick Bangala na Farid Mussa, kocha huyo msaidi alisema kuwa kwenye mazoezi ya leo ndio watajua kama wanaweza kuwatumia wachezaji hao kutokana na kutokuwa sawa siku za hivi karibuni.

“Kuna wachezaji kama Bangala na Farid wao bado hatujajua kama tutawatumia, kutokana na Farid kuumwa ghafla wiki hii na kukimbizwa hospital na Bangala nae aliumia siku mbili zilizopita mazoezi”- Aliongezea Kaze

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na rekodi ya kucheza mechi 18 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na mpaka sasa kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika klabu 16 zainazocheza Ligi.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Azam Fc ikiwa chini ya George Lwandamina walikubali kichapo cha mabao 2-0, dhidi ya Yanga, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kesho kwenye dimba la Azam Complex, utakuwa mchezo unaowakutanisha Azam FC na Yanga mara tatu kwenye uwanja huo, huku katika mara mbili Yanga akifanikiwa kuondoka na matokeo ya ushindi.

error: Content is protected !!