KUELEKEA mchezo wa awali wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Afrika, uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuwa huwenda ukawakosa wachezaji wake watatu kutokana na kukosa hati ya kimataifa ua uhamisho. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo…(endelea)
Mchezo huo wa hatua ya awali utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Septemba 12, mwaka huu ambapo Yanga itashuka dimbani dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Akithibitishja taarifa hiyo Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa mpaka sasa hati za wachezaji Khalid Aucho, Djuma Shabani na Fiston Mayele bado hazijatumwa kutokana na kuwepo kwa mivutano kwenye timu zilizotoka.
“Tutawakosa wachezaji wetu watatu, ambao ni Aucho, Mayele pamoja na Djuma Shabani”
“Kukosekana kwa wachezaji hawa haikuwa makossa ya klabu ya Yanga, Majele na Djuma Shabani mikataba yao ilikuwa inaisha tarehe 31, na tulipopeleka maombi ya hati zao waliatuambai tusubili hadi tarehe hiyo.” Alisema Manara
Aidha Manara alizungumzia kilichokwamisha hati ya usajili ya Aucho na kufungukuwa kuwa mchezaji huyo alikuwa kwenye migogoro na klabu yake aliyotoka nchini Misri hivyo walizuia kibali chake.
“Aucho alikuwa na mgogoro mkubwa na klabu yake, hakupewa mshahara wake kwa muda mrefu kidogo na baadae wakaenda Fifa wakaambiwa huyu ni mchezaji huru na wao wakashindwa kutupa hiyo hati kwa muda uliopangwa.”
Manara aliendelea kufafanua kuwa klabu hiyo, ilifanya juhudi ya kuwasiliana na Caf kuhusu hati za wachezaji hao, lakini hawajapata majibu yanayoweza kuwaruhusu wachezaji hao kucheza
“Tulifanya taratibu za kuwasiliana na watu wa Caf hawajatoa majibu ya kuwaruhusu wachezaji wetu kucheza, na tumeshawaandikia Fifa na tunaamini watatoa hati za wachezaji hao, kupitia Tff.” Alifunguka Manara
Wachezaji hao wote watatu wamesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili lililofungwa Agosti 31, na wataitumikia klabu ya Yanga, kwenye msimu ujao wa mashindano 2021/22
Leave a comment