
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Henry Mwaibambe
MFAWAMBO Mlengela (45) mkazi wa Kijiji cha Nyaurama, Kata Bugarama wilayani Ngara-Kagera, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumuua mke wake kwa kumpiga baada ya kujifungua watoto pacha. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).
Tukio hilo limetokea Machi 30 mwaka huu, ambapo marehemu Sinzobi Bialabawa (32), alijifungua watoto pacha wa kike, lakini mumewe akaanza kumpiga kwa madai kuwa katika ukoo wake ni ishara ya mkosi mwanamke kujifungua pacha wa jinsia moja.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Henry Mwaibambe, marehemu alipoteza maisha wakati akipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Ngara (Murugwanza) kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa ngumi na mateke.
More Stories
Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco
IGP Sirro: Hatufungui kesi za madai, migogoro ya ardhi
Panyabuku waanza kubaini TB