Saturday , 15 June 2024
Home Habari Mchanganyiko AU: Magufuli ameitingisha Afrika
Habari Mchanganyiko

AU: Magufuli ameitingisha Afrika

Mwenyekiti wa AU, Felix Tshisekedi
Spread the love

 

UMOJA wa Afrika (AU) umesema, kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, kimelitingisha Bara la Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo amesema na Mwenyekiti wa AU, Felix Tshisekedi, leo Jumatatu tarehe 22 Machi 20201, wakati anatoa salamu za rambirambi katika shughuli ya kitaifa ya kuuaga mwili wa Hayati Magufuli, katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Rais huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema, kifo cha mwanasiasa huyo, kimeliacha bara la Afrika yatima, kwani enzi za uhai wake alikuwa anapigania uhuru wake wa kiuchumi na kijamii.

“Kupotea na kuondoka kwa Hayati Magufuli kumetingisha bara zima la Afrika, Bara la Afrika linajikuta yatima kwa kupoteza mawanasiasa mkongwe aliyekuwa analenga kuboresha maisha ya watu wake, aliyekuwa pia analenga kutetea na kuendeleza uchumi wa kijamii na kiuchumi kwenye bara letu,” amesema Rais Tshisekedi.

Rais Tshisekedi amesema, AU itamkumbuka Hayati Magufuli kama mpiganaji, mzalendo aliyetimiza ndoto za waasisi wa Afrika, za kulifanya bara hilo kuwa na umoja baina ya watu wake.

“Tutabaki na kumbukumbu ya Hayati Magufuli ya mtu mpiganaji, mzalendo, sio tu kwa maslahi mapana ya Tanzania bali kwa umoja wa Afrika, mtetezi mkuu wa uhuru wa kitamaduni na kiuchumi wa Bara la Afrika. Aliyekuwa analenga kutimiza ndoto ya waasisi wa mataifa yetu kuleta umoja wa bara letu la Afrika na nchi zetu,” amesema Rais Tshisekedi.

Mwenyekiti huyo wa AU, amemuomba Rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, serikali yake na Watanzania kwa ujumla, kuendeleza mema aliyofanya Hayati Magufuli.

“Rais wa Tanzania, Watanzania kwa ujumla wimbi lililosababishwa na kifo cha hayati Magufuli, haitakiwi kamwe kupunguza dhamira yenu na nia yenu ya kuendeleza malengo yake, dira na dhima aliyokuwa nayo Hayati Rais Magufuli,” amesema Rais Tshisekedi.

Mwanasiasa huyo ametaja mambo mazuri yaliyofanywa na Hayati Rais Magufuli enzi za uhai wake serikalini, ambayo yanapaswa kuendelezwa, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma.

“Hii ni fursa kwenu kuja pamoja na kutimiza ndoto inayolenga kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii, tunapoongelea dhamira na dhima ya Hayati Magufuli, ninapenda kutaja kati ya mengi ambayo amefanya,” amesema Rais Tshisekedi

“Mapambano aliyoendesha dhidi ya ubadhirifu wa mali na fedha na rushwa, mambo ni kansa iliyokuwa inatafuna bara letu la Afrika na kuchelewesha maendeleo ya Afrika. Pamoja na kuimarisha msimamo wa demokrasia na kuifanya Tanzania nchi ya kuigwa barani Afrika.”

Aidha, Rais Tshisekedi amemtakia kheri Rais Samia katika majukumu yake mapya ya kuiongoza Tanzania kama rais.

“Nisingependa kuhitimisha bila kumtakia mafanikio makubwa Mama Samia, nikikutakia mafanikio makubwa kwenye nafasi hii mpya na kukuhakishia ushirikiano kutoka katika nchi yangu,” ameahidi Rais Tshisekedi.

Rais Samia amechukua madaraka ya urais baada ya Hayati Rais Magufuli kufariki dunia Jumatanoi ya tarehe 17 Machi 202i, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Hayati Rais Magufuli amefariki dunia kutokana na matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo. Mwili wake unatarajiwa kuzikwa Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, kijijini kwao Chato mkoani Geita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia apandisha kikokotoo kutoka asilimia 33-40

Spread the loveHATIMAYE Serikali imesikia kilio cha wastaafu wa utumishi wa umma...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Polisi wamtia mbaroni RC wa zamani aliyedaiwa kulawiti

Spread the loveJeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wafungwa, mahabusu ruksa kupiga kura

Spread the loveTUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa wafungwa,...

error: Content is protected !!