May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ATCL kufumuliwa upya

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Spread the love

 

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), linalojiendesha kwa hasara kwa miaka mitano sasa, litafumuliwa na kukabidhiwa kwa watu wenye weledi wa kusimamia. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Hiyo ni kauli ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan bungeni leo tarehe 22 Aprili 2021, wakati akilihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuwa rais tarehe 19 Machi 2021, baada ya kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021.

“Tutawekeza katika kupata rasilimali watu wenye uwezo na weledi wa kuliendesha shirika kibiashara. Na hii ina maana, tunakwenda kulifanyia uchambuzi wa kina na kuhakikisha tutakaowaamini kendesha shirika hilo, ni watu wenye weledi na wataweza kuliendesha kibiashara,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema, serikali yake itaendelea kuboresha usafiri wa anga, pamoja na utanuzi wa viwanja vya ndege kwenye mikoa mbalimbali na kujenga kiwanja kipya cha Kimataifa cha Msalato, Dodoma.

“Niseme tutaendelea kulilea shirika kimkakati ili liweze kujiendesha kiufanisi, na ninaposema kimkakati ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kutoa unafuu wa madeni na baadhi ya kodi na tozo kama inavyofanyika kwenye nchi nyingine.

“Shirika letu sasa hivi linasomeka ni shirika la deficit (hasara), halina thamani lakini ni kwa sababu ya kurithi madeni ya nyuma. Hivyo, kama sera tunakwenda kulitua mzigo wa madeni makubwa, lakini pia tutalipa unafuu wa kodi na tozo ili liweze kukua,” amesema.

error: Content is protected !!