August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ataka serikali isiwatelekeze wazee

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Spread the love

SAMSON Msemembo, mkurugenzi wa Shirika la kusaidia Wazee mkoani Morogoro (MOREPEO), ameitaka serikali kutimiza wajibu wake katika kulihudumia kundi la wazee ili kutatua changamoto zinazowakumba, anaandika Christina Haule.

Msemembo amesema hayo kwenye mafunzo ya afya ya macho yaliyoandaliwa na mradi wa Mwangaza, unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Conrad Hilton Foundation la nchini Uholanzi.

“Serikali ya awamu ya tano kuwatengea wizara wazee ambayo haikuwepo katika kipindi cha nyuma, inatufanya tuamini kuwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee zinaweza kutatuliwa kiurahisi,” amesema.

Ameongeza kuwa ugonjwa wa macho ni mojawapo kati ya magonjwa 10 yanayowasumbua wazee na kwamba iwapo watapata msaada juu ya tatizo hilo wataweza kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo.

Dk. Sencondri Njau, mratibu wa huduma ya macho mkoani hapa amesema baadhi ya matatizo ya upofu kwa wazee husababishwa na matumizi ya dawa za asili sambamba na matumizi ya dawa za macho pasipo kufuata ushauri wa daktari.

“Zaidi ya watu 22,000 wanaishi na ugonjwa wa macho mkoani Morogoro. Baadhi ya matatizo yao yanaweza kuzuilika au kutibika endapo watawahi hospitali kupatiwa tiba, tunawashauri wazazi kutozembea kupeleka watoto kupata chanjo hasa ya chanjo ya surua ambayo ni muhimu sana,” amesema.

error: Content is protected !!