October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aston Villa ya Samatta yabaki EPL

Spread the love

LIGI Kuu ya Uingereza (EPL) 2019/20 imehitimishwa huku ikishuhudia timu ya Aston Villa anayoicheza Nahodha wa Taifa Stars ya Tanzania, Mbwana Samatta ikinusurika kushuka daraja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Villa ikikuwa ilikuwa miongoni mwa timu tatu zilizokuwa hatiani kushuka daraja lakini sare ya 1-1 waliyoipata ugenini dhidi ya West Ham United imewafanya wasishuke.

Timu zilizokuwa zikichuana na Villa kushuka ambazo zimejikuta zikiaga ligi hiyo ni; AFC Bournemouth na Watford.

Licha ya kushuka daraja, AFC Bournemouth imehitimisha ligi hiyo kwa kuifunga Evetton 3-1 huku Watford wakikubali kipigo cha 3-2 kutoka kwa Arsenal.

Timu nyingine iliyoshuka daraja ni Norwich City.

Liverpool ndiyo mabingwa wa ligi hiyo huku nafasi ya pili ikishikwa na Manchester City, Manchester United ikiwa nafasi ya tatu na Chelsea ikiwa ya nne. Tizo hizo zote nne ndizo zitacheza michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya (Uefa).

Nafasi ya tano imeshikwa na Leiceter City na nafasi ya sita ikishikwa na Tottenham Hotspur huku Arsenal ikishika nafasi ya nane.

error: Content is protected !!