Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askou Gwajima agoma kukaa, ahojiwa akiwa amesimama wima
Habari za SiasaTangulizi

Askou Gwajima agoma kukaa, ahojiwa akiwa amesimama wima

Askofu Josephat Gwajima
Spread the love

 

MBUNGE wa Kawe, mkoani Dar es Salaam (CCM), Josephat Gwajima, ameendeleza mgomo wake wa kutotumia viti alivyopangiwa kutumia, wakati akihojiwa na Kamati ya Haki, Maadilina Madaraka ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Leo Jumatano, tarehe 25 Agosti 2021, akiwa katika Ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma, Askofu huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, aliamua kuhojiwa huku akiwa amesimama wima, baada ya kugoma kukaa katika kiti alichpangiwa kuketi.

Askofu Gwajima amehojiwa kufuatia tuhuma za kusema uongo na kushusha hadi ya Bunge, zinazomkabili.

Awali, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, alimkaribisha Askofu Gwajima aketi katika kiti kwa ajili ya mahojiano, lakini mwanasiasa huyo aligoma na majibizano yao yalikuwa hivi;

Mwakasaka: Karibu kwenye kiti

Askofu Gwajima: Ahsante

Mwakasaka: Karibu kwenye kiti au leo utasimama?

Askofu Gwajima: Leo nitasimama, nishazoea kusimama

Mwakasaka: Leo umeamua kusimama?

Askofu Gwajima: Naam mwenyekiti

Mwakasaka: Kwa nini hutumii kiti? Labda una sababu maalum? Naomab washa maiki au nayo tukubadilishie kama juzi?

Askofu Gwajima: Kama mnaweza sawa, lakini leo ni sawa

Mwakasaka: Leo ni sawa? kwa hiyo leo unatumia maiki hiyo tunakushuru. Sasa nilikuwa nakuuliza una sababu yoyote inayokufanya usikae kwenye kiti?

Askofu Gwajima: Niko comfotable kuongea nikiwa nimesimama.

Mwakasaka: Una tatizo lolote kiafya?

Askofu Gwajima: Kama itakupendeza.

Baada ya kauli hiyo ya Askofu Gwajima, Mwakasaka alianzisha kikao hicho cha mahojiano.

Akizungumza baada ya mahojiano hayo kumalizika, Mwakasaka amesema kamati hiyo imemaliza usikilizwaji wa shauri hilo na sasa inaendelea na kazi ya kufanya majumuisho ya kilichojiri katika mahojiano yale.

“Tumetoka kumalizia kumsikiliza shahidi wetu kwenye shauri la kwanza la Askofu Gwajima, ambaye nimemsikiliza. Amefika leo katika kamati hii ya maadili, tumemaliza shauri lake, tumeshamhoji na kwa kawaida kama kamati ikishamhoji na sasa inaendelea na kazi,” amesema Mwakasaka na kuongeza:

“Tuna majumusiho yetu tumeona nini, kamati inaendelea na kazi, lakini haizuiliwi tukiona kuna jambo la ziada kumuita, anaweza kuitwa wakati wowote, lakini tumemaliza shauri lake.”

Naye Askofu Gwajima, amesema mahojiano yake na kamati hiyo yalienda hivyo, hivyo anasubiri maamuzi yake, huku akisema atazungumza baada ya kamati hiyo kutoa kauli.

“Hali ya mahojiano iko sawa, kwa hiyo naisubiri kamati itawapa out come. Baada ya kamati kusema na mimi nitasema sababu sasa hii siwezi kusema chochote, naomba niwaachie kamati iseme,” amesema Askofu Gwajima.

Alipulizwa na wanahabari kwa nini aliamua kuhojiwa huku kasimama, Askofu Gwajima amejibu “nimependa kusimama leo, nimependa kuhojiwa hivi.”

Juzi Jumatatu, Askofu Gwajima aligoma kukalia kiti na kutumia maiki aliyopangiwa kutumiwa wakati anahojiwa na kamati hiyo, na kuiomba kamati hiyo imbadilishe vitu hivyo.

Baadae kamati hiyo ilimbadilishia kiti na maiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!