Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Askofu Shoo akemea ubaguzi nchini
Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Shoo akemea ubaguzi nchini

Askofu Dk. Fredrick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Spread the love

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi, kupandikiza chuki za ubaguzi wa kikabila. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kilimanjaro … (endelea).

“Kama kuna dhambi ambayo tunapaswa kujutia na kutubu, ni dhambi ya ubaguzi. Tusiruhusu watu kutuingiza kwenye dhambi hiyo,” alieleza Askofu Dk. Shoo.

Alisema, “hili nalisema hasa kwa ninyi viongozi vijana wa kisasa. Mnajifanya wajuaji sana. Tulieni. Mungu atawashusha.”

Baba Askofu Dk. Shoo alitoa kauli hiyo, wakati alipokuwa akiendesha ibada ya swala ya maombi ya aliyekuwa mwenuekiti wa makampuni ya IPP Limited, Dk. Reginald Mengi.

Askofu Dk. Shoo alikuwa akirejea kauli ya mwenyekiti  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chdema) na mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.

Katika salaamu zake mbele ya kadamnasi ya watu, Mbowe alisema, tabia ya baadhi ya viongozi nchini, kuchochea ubaguzi wa kikabila, kuwa ni hatari sana.

Mbowe alisema, ni muhimu kwa kila mmoja wetu, kukemea kauli za kibaguzi.

Alisema, “tuache kauli za kibaguzi. Tumuenzi Dk. Mengi, kwa vitendo. Mzee Mengi alikuwa mnyenyekevu na  alimpenda kila mmoja.

“Nashukuru Mhe. Ndugai uko hapa. Kazi ya Bunge ni kutetea maslahi ya wananchi. Teteeni maslahi ya wananchi mnaowawakilisha, kama kweli tunasema tumejifunza kutoka kwa Dk Mengi,” alisema askofu Dk Fredrick Shoo

Mbunge huyo wa Hai, mkoani Kilimanjaro – eneo ambalo Dk. Mengi anatokea – alisema, “ukimuona mtu anatoa kauli za kudai kuwa kabila fulani halisaidii walemavu, ujue taifa linakwenda kubaya.”

Amesema, tabia ya kibaguzi zinapaswa kukomeshwa, hasa kwa taifa ambalo limejijengea heshima ya kuwa wamoja kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati wa misa ya kumuaga Dk. Mengi leo tarehe 9 Mei 2019 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Moshi mkoani Kilimanjaro, Mbowe amesema, kitendo kutoa kauli za kibaguzi kilichofanywa na mtumishi mmoja wa serikali (hakutaja jina), kinapaswa kukemewa.

“Tusitengane kwa makabila yetu. Naomba wale wote walioguswa na kauli ile, nitoe msamaha kwa kumuaga Mzee Mengi,” amesema Dk. Mengi na kuongeza;

 “…anapotokea kiongozi mwenye mamlaka wakatoa kauli za kibaguzi, lazima tuungane wote kupinga,” amesema Mbowe ambaye, alianza kwa kuomba radhi kwa kauli hiyo.

Kwenye misa hiyo Mbowe alianza kwa kusema “niseme jambo moja ambalo limetukwaza wote, na kwasababu sina tabia ya unafiki, nitasema strait (moja kwa moja).

“Tuna nchi moja ambayo tunastahili kupendana, tunastahili kujengana, tunastahili kuheshimiana na tunastahili kumuona kila mmoja wetu ni sehemu halali ya nchi yetu.”

Amesema kuwa, hatua ya kuacha na kukubali kauli za kibaguzi, zitasababisha kupoteza utanzania wetu ambao ni moja ya sifa ya pekee.

“Tusikubali matendo na kauli za kibaguzi, zikatubagua katika nchi yetu, tukapoteza utanzania wetu, sifa ambayo tumejivunia kwa miaka mingi,” amesema.

Akimzungumzia Dk. Mengi aliyefariki tarehe 2 Mei 2019 Dubai, Falme za Kiarabu, Mbowe amesema, mfanyabiashara huyo mkubwa nchini alikuwa mnyenyekevu.

Na kwamba, alitoa misaada kwa watu anaowajua na asiowajua, hivyo kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa maisha ya Dk. Mengi.

Hata hivyo amesema, ni vema unyenyekevu unaooneshwa sasa katika kipindi hiki cha msiba, uoneshwe katika siku zote za maisha yetu.

“Kama ambavyo tumekuwa wanyenyekevu kwa kukaa pamoja kwa watu wa dini zote, kabila zote na vyama vyote, tuone basi unyenyekevu huu tunauendeleza katika maisha yetu yote ya kila siku,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!