Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Mwambapa: Spika ajaye aweke kipaumbele cha Katiba Mpya kwa Rais
Habari za Siasa

Askofu Mwambapa: Spika ajaye aweke kipaumbele cha Katiba Mpya kwa Rais

Spread the love

HUKU mchakato wa kumpata spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiendelea, imeshauriwa kupatikana spika mwenye ujasiri wa kumshauri Rais Samia Suluhu Hassan juu ya upatikanaji wa Katiba mpya. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma … (endelea)

Ushauri huo umetolewa leo tarehe 20 Januari, 2022 na Askofu Mkuu wa kanisa la Maombi na Maombezi kwa Mataifa yote (RUTACH), Living Mwambapa alipokuwa akizungumza na MWANAHALISIONLINE juu ya mchakato wa kumpata spika wa Bunge la Tanzania.

Askofu Mwambapa amesema nchi ya Tanzania kwa sasa inahitaji kuwa na katiba mpya ambayo inatokana nabmaoni ya wananchi na si vinginevyo.

Akizungumzia suala la kumpata Spika amesema kwa sasa inatakiwa kupatikana Spika mwenye ujasiri wa kumshauri rais ili aweze kuruhusu upatikanaji wa Katiba mpya kwa manufaa ya watanzania.

“Kwa sasa watu wanahamu sana ya kusikia nani atakuwa spika, lakini hata akipatikana spika miongoni mwao itakuwa ni yale yale kwani wanatembelea misingi ile ile.

“Ili kuwa na Bunge imara inahitajika kupatikana spika mwenye uthubutu wa kusimamia misingi ya katiba, kanuni na sheria na kutambua kuwa muhimili huo unatakiwa kufanya kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali bila woga na bila kuvunja sheria za nchi.

“Anatakiwa kupatikana Spika ambaye atatenda haki kwa wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao na mwenye kumshauri Rais bila uwoga kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya kweli kwa manufaa mapana ya taifa” ameeleza Askofu Mwambapa.

Akizungumzia umuhimu wa katiba mpya amesema itasaidia kila muhimili kufanya kazi kwa kujihamini bila kuingiliwa na itaweza kufanya kila kiongozi kufanya kazi kwa misingi inayotokana na katiba ya nchi.

“Tukiwa na katiba ya nchi itatoa mwongozo wa nini na nani anatakiwa kutimiza majukumu yake na kwa wakati gani na hiyo itasaidia mtu yoyote atakaye kuwa madarakani atafuata misingi ya katiba bila kujali itikadi ya chama anachokitumikia.

“Itasaidia kusimamia haki, kufanya kazi kwa usawa, upendo na udugu sambamba na kuhakikisha maendeleo ni haki ya kila mmoja awe na chama au asiwe na chama ilimradi ni mtanzania au anaishi Tanzania kwa utaratibu unaokubalika” amesema Askofu Mwambapa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!