ASKOFU wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula, madai ya upatikanaji katiba mpya, yanatakiwa yaende sambamba na uimarishwaji wa uhuru wa vyombo vya habari, ili visitumike ama kuminywa na vyama vya siasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Askofu Mwamakula ametoa kauli hiyo hivi karibuni, akihojiwa na MwanaHALISI Online na Tv, jijini Dar es Salaam.
“Miaka saba iliyopita vyombo vingi vya habari vilizimia, vingine vikawa mahututi, vingine vilipona na vilivyopona wakawa waoga kweli kweli. Katika ukombozi unaodaiwa sasa hivi wa katiba utaenda pamoja na uhuru wa vyombo vya habari ili visiweke mfumo na chama tawala au vyama vya siasa,” alisema Askofu Mwamakula.
Kiongozi huyo wa dini amesema, vyombo vya habari ni jicho na sikio la umma na nchi kwa ujumla, kwa kuwa vinafanya kazi inayogusa makundi yote iikiwemo Serikali.
“Kwa sababu hiyo chombo cha habari tukione kwamba ni mtumishi wa wote katika nchi, hakiko pale kwa ajili ya kufurahisha kundi fulani, hakiko kwa ajili ya Serikali wala chama tawala, upinzani au vyombo vya dini. Viko kwa ajili ya jamii yote kwa ujumla,” alisema Askofu Mwamakula.
Leave a comment