May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Mwamakula aitahadharisha CCM

Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Emmaus Mwamakula

Spread the love

 

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Emmaus Mwamakula, amekishauri Chama Cha Mapinduzi (CCM), kisikatae marekebisho ya katiba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Mwamakula ametoa ushauri huo leo Alhamisi tarehe 1 Julai 2021, katika uzinduzi wa kongamano la kidai katiba mpya, lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jijini Dar es Salaam.

“Waliokuwa kwenye madaraka sasa naomba watuelewe, hili jambo litawageuka na kama watakataa kubadili katiba kuna uwezekano upinzani kuingia madarakani kwa kutumia katiba hii na wakiitumia kulipiza kisasi itakuwa ole kwao, wataumia sana,” amesema Askofu Mwamakula.

Askofu Mwamakula amesema, endapo chama cha upinzani kitaingia madarakani kupitia katiba hiyo, CCM kitaathirika na mapungufu ya katiba hiyo.

“Tunataka tuwaambie wanaotawala kwamba katiba hii tunayoipinga, endapo wapinzani wakiingia kwa katiba hii watakwisha wote, lakini tukiibadilisha tutakuwa na kuheshimiana huko mbele,” amesema Askofu Mwamakula.

error: Content is protected !!