August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Lazaro kuitikisa Dar

Spread the love

EMMANUEL Lazaro, Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God ameandaa kongamano la uimbaji na uponyaji katika jiji la Dar es Salaam ambalo litashirikisha waimbaji maarufu wa injili wakiongozwa na Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Ambwene Mwasongwe na Kwaya ya Kinondoni Revival,anaandika Dany Tibason.

Waimbaji wengine watakaoshiriki katika kongamano hilo ni Kwaya ya Rivers of Joy International, Sarah Ndosi, Rapher James na Sam Yonah huku waumini wa madhehebu yote wakikaribishwa kwa ajili ya kupokea neno la uponyaji kutoka kwa askofu huyo mwenye heshima kubwa hapa nchini.

“Natoa wito kwa watu wote wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwani kutakua na maombi maalum kwa washiriki wote na kuna baraka za kipekee ambazo mtumishi huyu anaweza kuziachilia. Hii ni fursa adhimu ya kuhudumiwa na mtumishi huyu mkongwe katika masuala ya kiroho,” amesema Dk. Huruma Nkone Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG.

Dk. Huruma ambaye ndiye atakuwa mwenyeji wa kongamano hilo litakaloanza tarehe 19-23 Oktoba 2016 kuanzia saa 10:30 jioni katika Kanisa la Victory Christian Centre, lililopo Mbezi Beach A, Mwai Kibaki road amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika.

“Usafiri kwenda katika eneo la kongamano utapatikana katika vituo vya daladala vya Makumbusho, Mwenge na Bunju, kila mwenye fursa ya kufika na asikose kufika kwani watu wengi ambao hawamjui Askofu Lazaro ambaye amekuwa kiongozi wa kiroho wa miaka mingi hapa nchini,” amesema.

Askofu mstaafu Lazaro amekuwa akihubiri neno la Mungu kwa zaidi ya miaka 50.

error: Content is protected !!