September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Gwajima: Tumsapoti Rais Samia

Spread the love

 

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amewaomba Watanzania wamuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan, katika mkakati wake wa kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania, kupitia kipindi cha ‘Royal Tour’. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Gwajima ametoa wito huo leo Jumapili, akihubiri katika kanisa hilo, Ubungo mkoani Dar es Salaam.

Mbunge huyo wa Kawe, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema hatua hiyo ya Rais Samia inatakiwa iungwe mkono, kwani itaongeza idadi ya watalii pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa.

“Kitendo kinachofanywa na rais tukisapoti na tumshukuru Mungu Rais amefanya kazi kubwa, sekta ya utalii itapata watu, watajua tz tuna madini na vivutio vya utalii hii itaanyika uchumi wetu kwenda juu,”

“Kwa namna hiyo Rais anatakiwa atiwe moyo ili aendelee na hiyo kazi. Kazi ni ngumu na sisi tunamsapoti kwa nguvu zote,” amesema Askofu Gwajima.

Askofu Gwajima amesema, licha ya Tanzania kuwa vivutio vingi vya utalii, lakini hainufaiki kupitia rasilimali hizo, kutokana na kutojulikana ulimwenguni.

“Tanzania ni nchi nzuto lakini nje hatufahamiki sana na sababu hiyo tunakosa mengi, vivutio vingoi tunavyo lakino nje hawavijui. Rais ameamua mwenyewe awe mdau wa kuitangaza Tanzania katika mataia ya nje,” amesema Askofu Gwajima.

Askofu Josephat Gwajima

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya kuratibu mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa, Dk. Hassan Abbasi, Rais Samia ameanza kurekodi maeneo ya vivutio vya utalii na uwekezaji, Jumamosi tarehe 28 Agosti 2021 visiwani Zanzibar.

Mpango huo utakuwa endelevu ambapo Rais Samia anatarajiwa kuwatembeza wageni katika vivutio vya utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.

error: Content is protected !!