June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Gwajima, Silaa na Polepole wafika kuhojiwa CCM

Askofu Josephat Gwajima na Jerry Silaa wakisubiri kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM

Spread the love

 

WABUNGE wa Chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima wa Kawe, Jerry Silaa wa Ukonga na Humphrey Polepole wameitikia wito wa kufika kuhojiwa na kamati ya maadili ya chama hicho. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Askofu Gwajima na Silaa, wanahojiwa leo Ijumaa tarehe 3 Septemba 2021, makao makuu ya CCM jijini Dodoma na kamati hicho inayoongozwa na mwenyekiti wake, Hassan Mtenga.

Mbali na wabunge hao ambao wanatumikia adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge, mwingine ni Humphrey Polepole ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa.

Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Askofu Gwajima na Silaa tayari wamekwisha kufika na wanasubiri kuanza kuhojiwa huku Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho yeye amekwisha kuhojiwa na kuondoka.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!