Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima: Ninakwenda kupasua ukweli bungeni
Habari za Siasa

Askofu Gwajima: Ninakwenda kupasua ukweli bungeni

Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe
Spread the love

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dk. Josephat Gwajima amesema kesho tarehe 23 Agosti anakwenda kupasua ukweli mbele ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge baada ya kupokea barua ya wito wa kutakiwa kwenda kujieleza mbele ya kamati hiyo. Anaripoti Mwandishi wetu. (Endelea)…

Akizungumza mbele ya waumini wake leo Tarehe 22 Agosti, Askofu Gwajima amesema ameamua kuwaeleza umma kuhusu wito huo kwa kuwa aliyetoa barua hiyo ameisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema atakwenda mbele ya kamati hiyo na wategemee ukweli kama mojawapo ya imani ya CCM inavyosema kwamba ‘nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko’.

“Na nitaongezea mengine ambayo sijasema na mengine ambayo hamjasikia najazia. Ndio mtu wa Mungu anatakiwa kuwa hivyo, maisha yanatakiwa kuwa hivyo, lazima tusimamie nchi na watoto wetu.

“Ndio maana nasema namsapoti Rais, kamati ilisema watu wachanjwe au lah, na mimi nakuambia wewe kama rafiki yangu tumia hiyari yako uliyoambiwa uchanjwe au usichanjwe, sisi tumechagua lah.

“Kula matunda, fanya mazoezi, nenda kazini, ondoa uoga. Songa mbele, omba kwa dini yako. Mungu yupo hawezi kuacha tuondolewe namna hii,” amesema.

Jana tarehe 21 Agosti, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kupitia taarifa ambayo ilitolewa kwa umma, aliagiza Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa kufika mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwamo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya muhimili huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!