May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Gwajima atoa mpya bungeni

Askofu Josephat Gwajima

Spread the love

 

MBUNGE wa Kawe,kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima, amegoma kutumia kiti na kipaza sauti, vilivyopangwa kwa ajili ya kutumia akihojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tukio hilo lilitokea jana Jumatatu tarehe 23 Agosti 2021, bungeni jijini Dodoma, baada ya mwanasiasa huyo kuitwa ndani ya ukumbi, kuhojiwa na Kamati hiyo, kuhusu tuhuma zinazomkabili za kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Mhimili huo.

Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka, kumkaribisha Askofu Gwajima aketi, Mbunge huyo ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufunuo lililoko Dar es Salaam, alikataa na kuomba abadilishiwe kiti.

Fuatilia hatua kwa hatua ilivyokuwa kwenye mahojiano hayo katika Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Jumanne tarehe 24 Agosti 2021.

error: Content is protected !!