Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima akwepa swali la Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Gwajima akwepa swali la Rais Samia

Askofu Josephat Gwajima
Spread the love

 

Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima (CCM) amekwepa kujibu swali la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba atachaja au hachanji chajo ya Corona badala yake akajielekeza kuzungumza changamoto za jimbo lake. Anaripoti Mwandishi wetu.

Hayo yameibuka leo tarehe 2 Septemba 2021, Rais Samia aliposimama katika eneo la Tegeta na kuzungumza na wananchi wakati akielekea Bagamoyo kupiga picha za kutangaza utalii.

Akiwasalimia wananchi wa Tegeta na viunga vyake, Rais Samia alimkaribisha Askofu Gwajima kisha kuhoji; “mtachaja au hamchanji! Kisha wananchi wakajibu tutachanja.

Hata hivyo, Gwajima alipokaribishwa kuzungumza na wananchi alijielekeza kuzungumzia changamoto za jimbo hilo na kukwepa kujibu swali alilouliza Rais hasa ikizingatiwa Mbunge huyo ameweka wazi msimamo wake wa kutochanja chanjo ya corona.

Akizungumza katika mkutano huo, Gwajima alimshukuru Rais Samia kwa fedha zilizoelekezwa katika jimbo hilo kutekeleza miradi mbalimbali.

Rais Samia Suluhu Hassan

Alisema wana – Kawe si kwamba wanampenda Rais Samia pekee bali wana mahaba ya dhati kwake kwa kuwa amewafanyia makubwa jimbo hilo.

“Mama Samia ni rafiki yetu, aliwahi kufungua ofisi kule Mabwepande wakati akiwa makamu wa rais, lakini alipoingia madarakani kama Rais ametupendelea wana Kawe.

“Ametupatia bilioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa barabara 114 kupitia Tarura, lakini kuanzia tarehe 10,15 Septemba maji kutoka Ruvu chini yataanza kusambazwa kupitia matenki yliyojengwa,” alisema.

Alisema mbali na hayo, jimbo hilo linakabiliwa na uhaba wa shule hususani katika mtaa wa Wazo.

“Kule hakuna shule kabisa kuanzia msingi na sekondari… watoto wanakwenda kusoma Kunduchi na kuhatarisha maisha yao kwani wanagongwa na magari.

“Pia kuna suala la mafuriko, ulipokuwa ukigombea mwaka jana uliahidi bilioni 5 za kumaliza tatizo la mafuriko katika eneo la Chasimba, watu wengi wamepoteza maisha katika eneo hili, hivyo tunakukumbusha mama,” amesema Gwajima.

3 Comments

  • Ametumia hekima sana. Kuchanja na kutochanja ni hiari ya mtu huku akili yake mwenyewe Jumlisha na ushauri anaopata kutoka kwa jamaa zake, viongozi wake na kadhalika.

    Muda huo ulikuwa sahihi kuzungumzia matatizo na sio kuibua mvutano ambao umekuwepo kwa muda sasa.

    Rafiki yako,

    Aliko Musa

    Mbobezi Kwenye Ardhi Na Majengo

  • Ni dhahiri kuwa alikwepa kujibu suala la kuchanja. Ni kwa sababu hasira zake zote dhidi ya chanjo anazitoa akiwa anahubiri kanisani kwake. Hapo yeye ni simba. Lakini mbele ya mkutano wa rais kadamnasi anafyata mkia kwa kuogopa kuwa wananchi huenda wakamzomea. Unafiki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!