Mathias Issuja (87), aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma amefariki dunia jana usiku katika Hospitali ya Mtakatifu Gasper, Itigi mkoani Singida alipokuwa amelazwa, anaandika Wolfram Mwalongo.
Padri Raymond Saba, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) amethibitisha kutokea kifo hicho ambapo amesema, Askofu Isuja alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali yaliyochangia nwa umri wake mkubwa.
Askofu Isuja alistaafu mwaka 2005 akiwa Jimbo la Dodoma na kwamba, alipata daraja hilo takatifu mwaka 1972 ambapo aliwekwa wakfu na Hayati Kardinali Laurean Rugambwa.
More Stories
NMB yang’ara maonyesho ya Nanenane
Oman yavutiwa kuwekeza Tanzania
Waziri Madini: STAMICO imeingia kundi la wawekezaji