December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Dk. Shoo: Walah Rais Samia Mungu amekuweka kwa kusudi, kubali kuponya majeraha

Askofu Frederick Shoo, Mkuu wa Kanisa la KKKT

Spread the love

 

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kusimama katika yale aliyozungumza kwenye hotuba yake ya kwanza pamoja na kuendelea kuponya majeraha ya watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro …  (endelea).

Askofu Shoo ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Oktoba, 2021 katika ibada maalumu ya maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya Hospitali ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Rais Samia ambaye yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku mbili, ameshiriki katika maadhimisho hayo na kufungua mnara wa jubilee hiyo.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini amesema wakati wote atasema kweli kwamba Rais Samia Mungu amemuweka kipindi hiki kwa neema yake na kusudi lake.

“Ndio sababu nilitiwa moyo sana na ile hotuba yako ya kwanza ulipoapishwa kuwa Rais, uligusa mioyo ya watanzania.

“Tunajisikia kuheshimika sana kwa uwepo wako, sio sawa kwa sababu nafikiri hatujazoea sisi maaskofu na wakristo kusema, Walah! lakini napenda kukuambia Walah! Mungu amekuweka kwa kusudi… mama Mungu akuwezesha na asante kwa kuwa kiongozi wetu,” amsema Askofu Dk. Shoo.

Amesema Rais Samia amegusa mioyo ya watanzania hivyo anamkuhakikishia kuwa Watanzania wanampenda.

“Mungu akusaidie usimame katika nafasi yako, simama katika hotuba yako ya mwanzo, endelea kuponya jeraha za watanzania.

“Na kama mwenyewe ulivyokwisha kusema majina yako hayo yenyewe ni alama kutoka kwa Mungu, Samia Suluhu Hassan hakika naamini Mungu atakutumia na wewe uwe tayari kutumika hivyo hivyo.

“Watanzania wawe na ustawi maana yake afya njema pale ambapo wamejeruhika kwa sababu moja au nyingine, mama umruhusu Mungu akufanye uwe chombo cha kuponya watu jeraha zao,” amesema Askofu Dk. Shoo.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wenye mamlaka kusimama katika nafasi zao kwa uaminifu ili ahadi ya Mungu ya kuwarudishia taifa afya, ustawi wa kweli na kuponya jeraha upate kutimia.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Tujue tumewekwa kwa kusudi la Mungu kwa wakati huu, tuombe tutimize hayo mapenzi ya Mungu na daima tukumbuke kwamba tunao wajibu wa kuachia kama hao waasisi wetu walivyotuachia jambo la kukumbuka miaka 50 na sisi tuwe na kitu cha kuliachia taifa hili kukumbuka miaka 50 ijayo, kwa imani kwa kujitoa kwetu Mungu atatuwezesha wala sina wasiwasi,” amesema.

Hata hivyo, amewataka manabii, watawala, wataalamu wa tiba kutumia karama ambazo Mungu ameweka ndani yao.

“Naupongeza, na kuushukuru uongozi wa hospitali na wafanyakazi kwa kuwa mfano katika utoaji huduma,” amesema.

error: Content is protected !!