ASKOFU mkuu mstaafu nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu amefariki dunia leo Jumapili, tarehe 26 Desemba 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Tutu amefikwa na mauti akiwa na miaka 90 akikumbukwa kwa mapambano makubwa aliyoyafanya nchini humo ya ubaguzi wa rangi.
Alikuwa akisumbuliwa na saratani ya tezi dume aliyoipata mwishoni mwa mwaka 1990.
Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, Askofu Tutu aliyeipigania Afrika Kusini akiwa na Hayati Nelson Mandela, Rais wa Taifa hilo wa kwanza mweusi, alikuwa akilazwa mara kwa mara hospitalini.
Tutu alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984 ambapo Rais wa taifa hilo, Cyril Ramaphosa amesema, huo ni msiba mwingine mkubwa kwa Waafrika Kusini mashuhuri wakiondoka kwenye sura ya dunia.
Amesema, Askofu Tutu alikuwa mtu mashuhuri ndani na nje ya Afrika Ksuini, “kwetu sisi ametuachia urithi mkubwa uliokombolewa, utakaodumu vizazi hadi vizazi.”
Leave a comment