
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza akichanjwa chanjo ya corona
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe Mkoa wa Kagera, Dk. Benson Bagonza ametoa sababu kuu tatu, zilizomfanya kujitokeza kupata chanjo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (UVIKO-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).
Dk. Bagonza ametoa sababu hizo leo Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021, mara baada ya kumaliza kupata chanjo katika Hospitali teule ya Wilaya Karagwe (Nyakahanga).
Katika ukurasa wake wa facebook, Askofu Bagonza ametaja sababu hizo tatu kuwa ni; nimetafiti kwa madaktari wetu hapa nchini, USA, Ulaya na Canada. Nimeridhika na maelezo waliyonipa.
Pili, vita ya kibiashara kwa makampuni makubwa ni ya muda wote kwa bidhaa zote. Wanaokuuzia tishirt ya kuzuia risasi, kesho wanatengeneza risasi ya kupenya tishirt waliyokuuzia jana.
Askofu Bagonza ametaja sababu ya tatu ni chanjo ya Jensen inazuia kupata corona kwa asilimia 66. Ikitokea ukapata corona, chanjo hii inazuia kwa asilimia 86 usiingie katika ugonjwa mkali. Na chanjo hii inazuia kifo cha corona kwa asilimia 100.
“Mimi nimeridhika. Una hiari ya kuamua unavyopenda. Nimewahi kuugua corona kwenye wimbi la kwanza. Nimezika wengi. Ratiba yangu imejaa kwa wiki nzima mbele kwa ajili ya kuzika.
Nimechagua kufa kesho siyo leo,” ameema Askofu Bagonza
More Stories
Chongolo atoa siku 60 kwa MSD kupeleka vifaatiba hospitali Ushetu
NMB yafadhili wiki ya unywaji maziwa Katavi
#LIVE: Tuzo za EJAT2021, Majaliwa atoa ujumbe kwa MCT