Sunday , 29 January 2023
Habari za SiasaTangulizi

Askofu awavaa CCM

Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga amewakemea wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanazurura kutafuta vyeo badala ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutatua kero za Watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Mwamalanga ametoa karipio hilo jana tarehe 26 Novemba, 2022 wakati akizungumza na akinamama 100 wa CCM waliokwenda kuombewa dua, ili uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanyika kesho ufanyike kwa amani na salama.

Mwamalanga alisema matamanio yake ilikuwa kuona wana CCM wanamsaidia Rais Samia kwa kusimamia maagizo yake, lakini anachokiona wapo ‘bize’kutafuta dua za kupata uongozi na wengine wanatafuta kuwa Rais Samia baada ya mwaka 2025.

“Jifunzeni kwetu viongozi wa dini kutwa tunamuombea dua njema, lakini hatuishii kuomba tuu tunawasaidia Watanzania kwa kuchimba visima vya maji kupanda miti na kuelimisha wananchi kutunza misitu ya asili. Ukiuliza Askofu ni nani hapa bara na visiwani kule kwa Dk Hussein Ally Mwinyi, wananiita yule bwana mazingira kwa sababu kuhimiza upandaji miti.

“Ukifika kule Mbeya mjini watakuambia miti yote hiyo ni bwana mazingira Askofu Mwamalanga, lakini tupo pia bega kwa bega na vyombo vyake vya ulinzi na usalama kupambana na uingizaji wa dawa ya kulevya, ili kutimiza hitaji la Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana,” alisema.

Askofu huyo alisema wana CCM waliowengi wamejikita kumteta Rais Samia na kusaka madaraka tena kwa rushwa.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan

“Juzi Rais Samia amesema jambo la maana mno juu ya haki za Watanzania zinazokiukwa kwa sababu ya ubambikizwaji wa kesi kwa wanyonge. Leo CCM hamlisemi Samia amewaambia wanasheria madhara ya kuwabambikia watu kesi kunavyojaza watu magerezani na kupunguza nguvu kazi ya nchi.

Nilitegemea wanawake wa CCM mnahamasisha Watanzania kupenda haki kwa maandamano, lakini ninyi kutwa kutafuta vyeo ambavyo havitokani na haki ,”alisisitiza.

Askofu Mwamalanga alisema amesikitishwa na baadhi ya viongozi wa CCM kutwa wanajitahidi kujenga chuki kwa wananchi ili Rais Samia achukiwe na kwamba hiyo siyo sahihi hata kidogo ila ni kukosa ustaarabu.

Alisema Rais Samia ana dhamira njema ya kufikia ustawi wa pamoja na hataki kubagua watu kama baadhi yao wanavyopendelea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Askofu William Mwamalanga

Mwamalanga alisema Tanzania hatuna makaburu wakandamizaji na wakandamizwaji, ila bado CCM kuna watu wadumavu wa mawazo na akili ambao wanapenda viongozi wote wa vyama vingine wawe wanakamatwa na kuwekwa jela na hata kuuawa hiii ni hatari mno kwa watu wa jinsi hii.

Alisema kundi hilo likiona Rais Samia anatenda haki wanachukia, hivyo amewashauri waondokane na dhana hiyo na waende kuwa wajumbe sahihi.

“Tunauombea uchaguzi wa UWT uwe wa amani na furaha, wapatikane viongozi watakao msaiidia Rais Samia kuongoza Watanzania wote kula milo minne kwa siku siyo nusu mlo wa sasa …

“Leo hii wakulima wa kahawa mkoani Songwe, Wilaya ya Mbozi hawajalipwa fedha zao za kahawa tangu mwezi juni mwaka huu walipouza.

“Nendeni mkamwambie Rais hilo, pia mkamwambia figisu figisu za kule Mbarali ambapo maelfu ya wakulima wa mpunga wanafukuzwa kwenye ardhi yao kwa kizingizio cha uharibifu wa mazingira,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!