May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu awashukia Polisi “wananajisi kanisa”

Spread the love

 

ASKOFU mstaafu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Dk Glorious Shoo amekemea baadhi ya polisi kukosa weledi na kujua mipaka yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi … (endelea).

Amesema hivyo baada ya kuona baadhi ya walinzi hao wa usalama wa raia na mali zao wakifikia hatua ya kuingia makanisani wakiwa na bunduki.

Alisema hayo juzi Jumanne akifafanua, siku za karibuni kumezuka tabia hiyo ambapo baadhi yao wameingia makanisani wakiwa na silaha, kwa kinachodaiwa kwenda kuzuia wanaomwombea kiongozi wao, kisa wamevaa sare za chama cha siasa, na kwamba huko ni kuhatarisha usalama na kuvunja amani ya nchi.

Askofu huyo alisema kama lengo ni kukamata wanaokwenda kuombea kiongozi wao, zipo njia sahihi za kufuata, ambazo zingetumika lakini badala yake kinachoendelea sasa, ni sawa na kulinajisi Kanisa, jambo ambalo halikuzoeleka huko nyuma.

Undani wa habari hii soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Ijumaa tarehe 20 Agosti 2021.

error: Content is protected !!