May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu awaonya wanaojipendekeza kwa Rais Samia

Spread the love

 

PETER Konki, Askofu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), amewataka wanasiasa nchini humo, kuacha kujipendekea kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ili waweze kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Askofu Konki, ametoa kauli hiyo leo Jumapili tarehe 18 Aprili 2021, katika ukumbi wa Chimwaga, mkoani Dodoma, kwenye kongamano la kuombea Taifa na kumshukuru Mungu kwa maisha ya Hayati Rais John Pombe Magufuli na kumwombea Rais Samia.

Hayati Magufuli, alifikwa na mauti akiwa madarakani, tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Kongamano hilo, limehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa dini na kiserikali wakiwemo, Rais Samia na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi.

Askofu Konki amesema, kumekuwa na wanasiasa wanaokashfu utumishi wa Hayati Magufuli na kumsifia Rais Samia kwa maslahi binafsi ya kutaka kuteuliwa.

“Nimeona kwenye mitandao ya kijamii wanasiasa wakimsifia Rais Samia na kumkashfu Hayati Magufuli, hii ni kujipendekeza ili wateuliwe kwenye nafasi mbalimbali, huu ni unafiki mkubwa sana,” amesema Askofu Konki, huku akishangiliwa na wahudhuliaji wa kongamano hilo

Amesema, Hayati Magufuli “ni kipenzi cha wengi hivyo wanasiasa wasituganyanywe.”

error: Content is protected !!