November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askofu atoa elimu kwa wapiga kura

Spread the love

MAKAMU wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Chesco Msaga, amewataka watanzania kushiriki uchaguzi mkuu na kuwachagua viongozi wanaowataka kwa utulivu na amani kwa kufuata misingi aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Msaga alitoa rai hiyo jana wakati akitoa mahubiri kwenye ibada maalumu ya kumuombea hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Nyerere mjini hapa.

Makamu huyo wa askofu amesema kuwa watanzania hawana budi kuishi kutokana na misingi aliyoicha Mwalimu Nyerere ambayo ni amani na mshikamano ambao ndiyo tunu kubwa kwa taifa letu.

Amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu watanzania wanatakiwa kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi wanayemtaka bila kuharibu amani na mashikano aliouenzi baba wa taifa wakati wa uhai wake.

“Tusiharibu kabisa misingi aliyoweka Baba wa taifa kwa kutaka madaraka kwa fujo au kufanya fujo ili kuweza kujipatia sifa za kisiasa, hivyo basi niwasihi kuhakikisha amani utulivu na mashikano aliyoiweka baba wa taifa tunailinda katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kushiriki katika kupiga kura bila ya kumbuguzi mtu,” amesema Msaga.

Aidha amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuiga mambo mengi aliyokuwa kiyafanya baba wa taifa ikiwa ni pamoja na kutokuwa na tabia ya kujilimbikizia mali kama ilivyo kwa baadi ya watu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, akitoa salamu za mkoa katika ibada hiyo amesema kuwa watanzania wataendelea kumkumbuka Baba wa taifa kwa mambo mengi ambayo aliyafanya wakati wa uhai wake kwa kuwafanya wawe wamoja.

“Leo tuazimisha kifo cha baba yetu wa taifa Mwalimu Nyerere lakini tutaendelea kumkumbuka kwa mambo mengi aliyotufanyia wakati wa uhai wake ambayo na sisi tunatakiwa kuyaishi ili kuweza kendeleza amani na mshikamo aliouacha,” amesema Gallawa.

Katika ibada viongozi wengine walioshiriki ni Spika wa Bunge, Anna Makinda, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Fenela Mukangala, Katibu Mkuu Tamisemi, Jumanne Sagini pamoja na makatibu tawala na wakuu wa Wilaya mbalimbali.

error: Content is protected !!