IKIWA imebaki siku moja Serikali kuwasilisha Bajeti Kuu bungeni, Askofu wa Kanda ya kati wa makanisa la Baptist, Antony Mlyashimba ameitaka ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha bajeti hiyo inalenga kuinua kipato cha Watanzania. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).
Pia ametoa wito kwa serikali kupunguza matumizi ya anasa kama vile kununua magari ya bei ghali, kupunguza misafara ya viongozi wa kuu wa serikali na hata safari za nje ili kubana maumizi.
Askofu Mlyashimba ametoa wito huo jana tarehe 12 Juni, 2022 muda mfupi baada ya kumaliza kuhudumia ibada maalum ya shukrani na kushiriki meza ya Bwana katika kanisa hilo.
Aidha, ameishauri serikal kuwekeza zaidi katika masuala ya uzalishaji katika sekta za kilimo, afya, elimu pamoja na mifugo.
Kiongozi huyo wa kiroho amesema serikali inatakiwa kuwa na vipaumbele vichache lakini vinavyotekelezeka badala ya kuwa na vipaumbele vingi ambavyo havitekelezeki.
“Pia serikali itoe ruzuku katika sekta ya kilimo ili kukuza uzalishaji.
“Kuna kila sababu ya kuhakikisha Tanzania inaruhusu uwepo wa uraia pacha jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi na kuwafanya watu waliopo nchi za nje kurudi na kuwekeza ndani,” amesema.
Leave a comment