July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu akemea ‘wachungaji feki’ wanaoharibu Ukristo

Spread the love

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Light House Christian Center Dar es Salaam, Dk. Rejoice Ndalima amewakemea baadhi ya watu ambao wanajiita watumishi wa Mungu lakini wamekuwa wakitenda vitendo viovu na kuutukanisha Ukristo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbali na kuutukanisha Ukristo Askofu huyo alisema kuwa kwa sasa baadhi ya jamii imekosa kabisa imani na watumishi kutokana na kufanya matendo machafu ambayo hayalingani na utumishi wao.

Dk. Ndalima kuwa hivi sasa jamii imekosa imani na watumishi wanaotunukiwa kutokana na kukosekana kwa vitendo vibaya tofauti na jinsi ilivyokusudiwa na tuzo hiyo ambayo inatolewa kwa lengo la kuwataka kuitumia jamii kwa kuwaonyesha maadili mema ya kiroho na siyo kwa kuwakemea wanaowaongoza.

Awali askofu huyo akihubiri kwenye sherehe ya kutunuku tuzo za utendaji uliotukuka kwa watumishi hao wapatao 42 wa kada mbalimbali kwa maana ya Viongozi wa Dini, Serikali na Taasisi mbalimbali.

Alisema kuwa siyo busara kwa viongozi ambao wanatakiwa kuwa kioo cha jamii kujiingiza katika matendo mbayo yanajengewa mashaka na wale wanaowazunguka.

Naye Mchungaji kiongozi wa kanisa la Evangelisct Assembelise of God Tanzania (EAGT), Ipagala Dodoma, Evance Chande amewataka watanzania kufanya kazi  kwa bidii ili kuiunga juhudi zinazofanywa na serikali katika malengo yake ya kufkia uchumi wa viwanda vya kati kama ilivyokusudiwa na jitihada hizo na Rais John Magufuli.

Chande amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe ya kuwatunuku watumishi mbalimbali wa kiroho, kijamii na taasisi kiraia na kiserikali waliofanya vizuri  tuzo ya  utendeji  uliotukuka iliyotolewa na taasisi ya Outreach Care yenye makao yake hapa nchini Tanzania.

Akizungumza baada ya kutunukiwa watumishi hao tuzo hiyo alisema kuwa ili tuweze kufikia malengo ya rais wa awamu ya tano,ni muhimu watanzania wakafanyaka kazi kwa jitihada na kujituma  kwa ajili ya kufkia hatua hiyo ya uchumi utakaotuwezesha  viwanda hivyo vya kati.

“Leo hapa tumeshuhudia watumishi hao wakipatiwa tuzo hii iliyotolewa na Outreach Care wamepewa kutokana na juhudi zao walizozifanya ambazo zimelenga kwa ajili ya kuunga jitihada ya kumuunga mkono Rais wetu pamoja na kuwa walio wengi ni watumishi wa mungu ambao pia kwa kazi yao haina tofauti katika jitihada hizo za kufkia uchumi wa viwanda vya kati,” alisema.

Naye Askofu wa Wolrd Ministres, Damas Thadey kwa upande wake amewataka vijana kujituma katika utendaji wa kazi ili na wao waweze kutunukiwa tuzo mbalimbali ambazo zitakazowafanya kutambulika kiroho,kijamii na hata kwenye serikali.

Alisema kuwa changamoto iliyopo kwa vijana walio wengi wamekuwa hodari kwa kuionyoshea serikali vidole huku wakiishi bila kufanya kazi, hatua ambayo itawafanya kuendelea kulalamika na kushindwa kuchangia maendeleo ya Taifa lao.

error: Content is protected !!